Header Ads Widget

TANZANIA YAPOTEZA KIONGOZI MKONGWE JENISTA MHAGAMA

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

TANZANIA imeingia katika kipindi cha msiba mkubwa leo baada ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho na Waziri wa zamani Jenista Joakim Mhagama aliyefariki akiwa na umri wa miaka 58 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma .

Kifo hiki kimesikitisha si tu familia na marafiki wa karibu bali pia wananchi wa Peramiho na wabunge wenzake Spika wa Bunge la Taifa Mussa Azzan Zungu ametoa taarifa rasmi akisema tumepoteza kiongozi mwadilifu mchapakazi na mzalendo wa taifa kifo cha Mhagama ni pengo kubwa kwa Bunge na kwa wananchi aliowahudumia kwa dhati. 

Viongozi mbalimbali wa Serikali wameanza kuwasili nyumbani kwa marehemu eneo la Itega jijini Dodoma kutoa salamu za pole kufuatia kifo chake cha ghafla kilichotokea asubuhi ya leo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule

Akizungumza mara baada ya kuwasili amesema marehemu atakumbukwa kwa namna alivyolitumikia Taifa katika wizara mbalimbali alizowahi kuhudumu amesema pia marehemu alikuwa kiongozi mchapakazi mnyenyekevu na mwenye kujituma aliyeonyesha uzalendo na uadilifu katika nafasi zote alizokabidhiwa

Jenista Mhagama alijulikana kwa uchapakazi ucheshi na heshima kwa wakubwa na wadogo Kabla ya kuingia siasa kikamilifu alifanya kazi kama mwalimu jambo lililoendeleza uhusiano wake na wananchi na kuifanya siasa kuwa ya karibu na mahitaji ya jamii. 

Alihudumu katika nafasi mbalimbali serikalini zikiwemo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu akihusika na sera bunge ajira vijana na watu wenye ulemavu Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora akisisitiza uwajibikaji na ufanisi serikalini na Waziri wa Afya kuanzia Agosti 2024 akisimamia sekta ya afya nchini .

Prof Riziki Shemdoe Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI amesema marehemu Jenista Mhagama alikuwa kiongozi wa kipekee aliyejulikana kwa uwezo wake wa kuelekeza na kushirikiana na viongozi wengine wa ngazi za chini kwa urafiki bila kuwapa msongo wa mawazo 

Aidha ameeleza kuwa mchango wa marehemu katika maendeleo ya jamii na katika kutekeleza sera za Serikali utaendelea kuenziwa huku akisisitiza kuwa mfano wake wa uadilifu na uongozi wa busara utabaki kuwa kielelezo cha kuigwa na viongozi wengine na kizazi kijacho

Rais Samia Suluhu Hassan kupitia ujumbe wa rambirambi alieleza msikitiko wake mkubwa na kutambua mchango wa Mhagama katika siasa na huduma ya umma Rais alisisitiza kwamba Mhagama alikuwa kiongozi wa mfano mwadilifu na mnasihi wa wananchi wengi

Ofisi ya Bunge na familia ya marehemu zinaandaa mpango wa mazishi ambao utatangazwa hivi karibuni Wanafunzi wa Mbunge Mhagama wanasiasa wenzake na wananchi wa Peramiho tayari wameshatoa salamu za pole na kumbukumbu za kiongozi aliyekuwa chimbuko la ushawishi mzuri na maendeleo

Hata hivyo marehemu Jenista Mhagama ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya taifa uongozi thabiti na uhusiano wake wa karibu na wananchi

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI