Header Ads Widget

RAIS SAMIA AYASHUKIA MATAIFA YANAYOIPANGIA TANZANIA LA KUFANYA " WHO ARE YOU?

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Tanzania ni huru na haitoingiliwa na serikali ama chombo kingine chochote kutoka nje ya Tanzania, akisema fedha chache wanazozitoa kwa Tanzania si kigezo cha kuingilia mambo ya Tanzania.

Dkt. Samia ameyasema hayo leo Jumanne Disemba 02, 2025 Jijini Dar Es Salaam alipozungumza na wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, akisisitiza kuwa Tanzania imeumbwa vizuri na kuwekwa pazuri katika soko na siasa za dunia na ndilo tatizo linalosababisha kupigwa vita.

"Nje huko wanakaa kuwa Tanzania ifanye hili na hili halafu ndiyo itakuwa hivi, who are you? Niwaulize ndugu zangu, kwao hayatokei? Tumenyanyua sauti sisi kusema ya kwao? Wanadhania kuwa bado wao ni master wetu, ni wakoloni kwetu? Kitu gani? Ni fedha chache wanayotugaia? Na fedha yenyewe sasa hivi haipo, tunafanya biashara wao wapate na sisi tupate." Amekaririwa Rais Samia.

Rais Samia amesema Tanzania kutofungamana na upande wowote pamoja na uwepo wa rasilimali nyingi ikiwemo bahari, madini na Maziwa kumeifanya Tanzania kuwa muhimu kiuchumi duniani suala ambalo limewanyima usingizi Mataifa mengi duniani.

Rais Samia amewaambia watanzania kuwa maumbile na Utajiri wa Tanzania ni muhimu kila mmoja kutoruhusu kuwa laana na sababu ya Watanzania kuuana kwa kushawishiwa na wanaoitolea macho Tanzania, akisisitiza kuwa huu ni wakati muhimu wa kushikamana na kuendeleza umoja wa Watanzania.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI