Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba, amesema kuwa michakato yote ya ununuzi wa mali za umma nchini ni lazima izingatie Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2024, huku PPRA ikiwa msimamizi mkuu wa utekelezaji wa sheria hizo.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ilifanikiwa kupitisha sheria hiyo baada ya kupokea maoni mengi kutoka kwa wadau mbalimbali, wakiwemo wabunge, jambo lililosaidia kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika sekta ya ununuzi wa umma.
Simba ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma katika semina iliyoandaliwa na PPRA ambapo lengo la semina hiyo lilikuwa ni kuwapatia waandishi wa habari uelewa mpana kuhusu sheria ya ununuzi wa umma, ili waweze kuandika taarifa kwa usahihi na kusaidia kutoa ufafanuzi pale panapotokea upotoshaji.
" Utoaji wa semina hii ni sehemu ya mwendelezo wa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa ununuzi wa umma, kwani waandishi wa habari ni wadau muhimu na nguzo ya msingi katika kuimarisha ununuzi bora na wenye tija nchini Tanzania, " Amesema









0 Comments