Madiwani wa manispaa ya Kigoma Ujiji wakiwa kwenye kikao cha kwwnza cha baraza baada ya kula kiapo
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WAJUMBE wa baraza la madiwani la manispaa ya Kigoma Ujiji wamemchagua kwa kauli moja Diwani wa kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji Mussa Maulid kuwa Meya wa manispaa hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Kisena Mabuba (mbele) akimuongoza Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji Mussa Maulid kuingia kwenye kikao cha kwanza cha baraza la manispaa ya Kigoma Ujiji baada ya madiwani kuapishwa na kufanya uchaguzi wa meya na Naibu Meya
Maulid amechaguliwa kuwa meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kupata kura 24 za ndiyo kati ya kura 25 za madiwani waliohudhuria baraza hilo ambapo mgombea huyo alipata kura moja ya hapana.
Diwani wa kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma akishukuru baada ya kuchaguliwa na madiwani kuwa meya wa manispaa hiyo
Akitangaza matokeo hayo Afisa Tawala kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya Kigoma, Dollar Buzaire alimtangaza Mgeni Kakolwa kuwa Naibu Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kupata kura 24 za ndiyo na kura moja ya hapana.
Afisa Tawala ofisi ya Mkuu wa wilaya Kigoma Dolla Buzaire (aliyesimama) akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji




0 Comments