Na Matukio Daima Media, Iringa
Mkwawa Jogging Club imeendelea kuwa moja ya club bora na yenye mvuto mkubwa jijini Iringa, ikiwa na dhamira ya kuhamasisha jamii kupenda mazoezi, hasa matembezi na kukimbia (jogging), kama sehemu muhimu ya kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.
Club hii imekuwa mfano halisi wa namna wananchi wa kawaida wanavyoweza kubadilisha maisha yao kwa kuwekeza katika mazoezi bila gharama kubwa.
Katika miaka ya hivi karibuni, Serikali imekuwa ikisisitiza umuhimu wa mazoezi kwa makundi yote katika jamii ili kupunguza ongezeko la maradhi kama kisukari, shinikizo la damu, unene uliopitiliza na magonjwa ya moyo.
Mkwawa Jogging Club imekuwa mstari wa mbele kutafsiri kwa vitendo wito huo wa serikali kwa kuandaa mazoezi ya pamoja kila wiki, kushirikiana na wakazi wa maeneo mbalimbali ya Iringa, na kuwahimiza vijana, watu wazima na hata wazee kushiriki ili kuimarisha afya zao.
Club hii imejijengea umaarufu kwa kasi kutokana na nidhamu, umoja na ratiba zake bora za mazoezi zinazowavutia watu wa kada mbalimbali.
Wengi waliowahi kujiunga na mazoezi haya wanasema kuwa Mkwawa Jogging imekuwa zaidi ya club ni familia pana inayojenga afya, urafiki, kujiamini na kuongeza hamasa ya kujipenda.
Licha ya mafanikio, changamoto bado zipo
Pamoja na mafanikio haya, Mkwawa Jogging Club bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa vya mazoezi.
Vifaa kama furana za wakimbiaji, track suits, begi za mazoezi, viatu imara vya jogging na vifaa vya kujikinga na baridi au jua bado ni mahitaji yanayohitajika kwa uharaka.
Changamoto hii imeibua fursa pana kwa wafanyabiashara, wadau wa michezo, makampuni ya bidhaa, na watoa huduma mbalimbali kutumia Mkwawa Jogging Club kama jukwaa la kujitangaza.
Kupitia udhamini wa vifaa vya mazoezi kama furana, tracksuits au kofia zenye nembo ya mdhamini, kampuni au mjasiriamali anaweza kufikiwa na maelfu ya watu ndani na nje ya Iringa.
Popote wanapofika wanachama wa Mkwawa Jogging, nembo ya mdhamini huonekana na kuendelea kulitangaza jina lake.
Kwa sasa, club imekuwa ikihudhuria matukio mbalimbali, kukimbia katika barabara za Iringa na mikoa jirani, jambo ambalo linatoa fursa kubwa kwa mdhamini yeyote kupata matangazo ya kitaifa bila gharama kubwa.
Matukio Daima Media yatoa mchango mkubwa
Katika kuhakikisha jitihada za Mkwawa Jogging Club zinatambulika zaidi, chombo cha habari cha Matukio Daima Media kimekuwa mshirika mkubwa katika kutangaza na kufuatilia maendeleo ya club hiyo.
Kupitia habari, picha na video zinazotolewa mara kwa mara, jamii imezidi kufahamu kazi nzuri inayofanywa na club, jambo ambalo limeongeza mwitikio wa watu wengi kujiunga.
Matukio Daima Media imekuwa daraja muhimu kati ya club na wananchi, kwa kuibua vipaji, kuhamasisha ushiriki wa vijana, na kutoa taarifa zinazoonyesha thamani ya mazoezi katika kujenga taifa lenye afya bora.
Hivyo, jitihada hizi zimekuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa club pamoja na kufungua nafasi kwa wadau wengine kushirikiana nayo.
Mwito kwa jamii kujiunga
Kwa kuangalia mafanikio yaliyoonekana ndani ya kipindi kifupi, Mkwawa Jogging Club inatoa mwito kwa wananchi wa Iringa na maeneo ya jirani kujiunga na familia hii ya mazoezi.
Kujiunga ni bure, na faida ni nyingi kuanzia kuboresha afya, kupunguza msongo wa mawazo, kujenga mahusiano mapya, kuongeza furaha na hata kujiamini zaidi.
Club hii inaendelea kukua kila siku, na kwa ushirikiano wa wadau pamoja na nguvu ya Matukio Daima Media, kuna matumaini makubwa kuwa itafikia hatua ya kuwa club ya mfano nchini Mkwawa Jogging Club ni ishara ya mabadiliko chanya katika jamii mabadiliko ya mtazamo, tabia na afya.
IWAPO UNAHITAJI KUJIUNGA AMA KUIDHAMINI MKWAWA JOGGING CLUB PIGA SIMU 0762 517 031/0717459399







.jpg)






0 Comments