Mwaka 2019 Alaah Salah alikuwa na umri wa miaka 22 huku akiwa mwanafunzi wa mwaka wa pili kwenye Chuo Kikuu cha Sudan. Aliongoza na kuhamasisha maandamano yaliyomtoa Omar Bashir madarakani. Mpaka sasa Omar Bashir yuko kifungoni akitumikia adhabu ya makosa ya jinai aliyotenda madarakani.
Wakati huo wengi waliingizwa barabarani bila ya kujua kuwa walikuwa wakifanikisha mradi wa aliyeitwa mwanamke shujaa na mzalendo, Salah akapata umaarufu mkubwa, akitukuzwa na Mataifa na Vyombo vya habari vya Kimagharibi, akitwikwa majina kadhaa na kumpa sifa za ujasiri na ushujaa kama mpigania haki, demokrasia na Mwanamapinduzi wa kweli.
Baada ya Mapinduzi ya mwaka 2019 upepo ukabadilika, lengo la mabeberu likatimia, Omar akapinduliwa watu wakidhani kuwa matumaini yao yanaenda kutimia, bahati mbaya ndio ukawa mwanzo wa kuiharibu nchi yao wenyewe, Jinamizi la mauaji likatanda, unyanyasaji ukatapaaa Sudan na Mwanamke Salah akapotea na haonekani tena akikemea ama kupaza sauti kuhusu unyanyasaji na ukatili unaoendelea nchini mwake.
Taifa hilo limekumbwa na moja ya migogoro ya kibinadamu mibaya zaidi duniani, zaidi ya watu milioni 15 wamelazimika kukimbia makazi yao na zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada wa kibinadamu, wakiwemo milioni 24.6 wanaokabiliwa na njaa kali, kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa. Makadirio yanaonesha kuwa watu wapatao 150,000 wameuawa ndani ya mwaka wa kwanza wa mapigano pekee.
Alaah ni mfano halisi wa kile Mange Kimambi anachokifanya kwa sasa nchini Tanzania, haishi Tanzania na mara zote amedai kuwa hana la kupoteza nchini. Si ndugu wala mali zake na ndicho kinachomfanya kuwa kinara wa kuhamasisha vurugu nchini- aiweke nchi kwenye janga, apokee malipo yake na atuache Watanzania tukitaabika katikati ya machungu ya kuiharibu nchi yetu wenyewe.
Watanzania tuamke, tujifunze kwenye tone dogo la maumivu tulilolipata Oktoba 29, 2025. Tujiepushe na akina Alaah wa Tanzania wanaobebwa na kusifiwa na Vyombo vya habari vya magharibi ili kutupofusha akili na kuamini kuwa wanatutakia mema ilihali wanasimamia maslahi yao binafsi.








0 Comments