Header Ads Widget

MHANDISI MAHUNDI AITAKA TICD TENGERU KUWEKA MIPANGO ENDELEVU


Na,Jusline Marco;Arusha

Naibu waziri Maendeleo ya Jamii,jinsia, wanawake na makundi maalum Mhandisi Maryprisca Mahundi ameitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuweka mpango endelevu wa kuendelea wanafunzi wabunifu na wenye vipaji.

Akizungumza Disemba 5, 2025 katika maafali ya 15 duru ya 2 mwaka 2025  ya chuo cha maendeleo ya Jamii Tengeru,ambapo alisema Wizara inakiangalia chuo hicho kama Taasisi ya kimkakati katika kuinua hali ya maisha ya watu kwani sekta ya Sanaa, ubunifu kwa sasa inaweza kuajiri wahitimu wengi kutokana na ukuwaji wa Teknolojia.

Aliongeza kuwa mabadiliko makubwa na yenye kasi katika ukuaji wa mapinduzi wa Teknolojia,mabadiliko ya kiuchumi yanayolazimiaha kuibuka kwa sekta ikiwemo sekta ya ubunifu na Sanaa ,kijani na blue, mabadiliko ya tabia nchi na mabadiliko ya kijamii kutokana na muingiliano wa jamii zenye fikra ,mahitaji na mitazamo tofauti kunaleta changamoto ambazo hazikuzieleka hapo awali hivyo yanaleta fursa mpya ambazo zinaweza kusaidia katika jamii.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt.Bakari George katika maafali hayo mbali na wito alioutoa kwa wahitimu hao na kueleza baadhi ya mafanikio katika Taasisi hiyo amesema kuwa chuo hicho kinatambua umuhimu wa ubunifu na ujasiriamali katika kupunguza utegemezi wa wahitimu.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri Mahundi,  Mwenyekiti wa Bodi ya muendeshaji TICD Dkt. John Lusingu amesema pamoja na mafanikio yote ya Taasisi hiyo,ameiomba Bodi ijayo kushughulikia upatikanaji wa hati miliki wa ardhi,ukamilshaji wa mchakato wa kuunganisha Taasisi na vyuo vya maendeleo ya Jamii na maendeleo ya Jamii ufundi,mabadiliko ya sheria ya uanzishwaji wa Taasisi ,mageuzi katika matumizi ya Teknolojia pamoja na akili unde  sambamba na upatikanaji wa fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.

Ameongeza kuwa Bodi ya Muendeshaji ni kiungo muhimu katika uongozi wa Taasisi yoyote ya Umma na ni chombo chenye wajibu wa kusimamia utekelezaji wa majukumu ya kiutawala, kimkakati na kifedha ili kuhakikisha uadilifu,uwajibikaji na uendelevu wa Taasisi kwa ajili ya kuongeza tija na kuchochea kiwango cha utoaji wa huduma.

Hata hivyo jumla ya wanafunzi 1813 kati yao wanaume wakiwa 757 sawa na asilimia 41.8   na wanawake 1056 sawa na asilimia 58 wamefuzu na kutunukiwa tuzo za shahada ya uzamili,shahada ya kwanza, stashahada na Astashahada za Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ambapo kati ya wahitimu wote, wahitimu 92 wametunukiwa shahada ya uzamili,wahitimu 305 wametunukiwa shahada ya kwanza,wahitimu 427 wametunukiwa stashahada, wahitimu 432 wametunukiwa Astashahada na wahitimu 553 Astashahada ya msingi.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI