Header Ads Widget

MAZINGIRA PLUS YAZINDUA MRADI WA TAKA SIFURI KWA SHULE ZA MSINGI SITA DAR

 

TAASISI ya Mazingira Plus yazindua mradi wa Taka Sifuri shuleni ambayo itahakikisha inatunza mazingira kwenye maeneo ya shule za msingi nchini lakini kwa kuanzia katika shule sita za jiji la Dar es salaam.


Akizungumza katika warsha ya kufungua mradi huo, Dar es Salaam, Mratibu wa Mazingira Plus, Suleiman Mang’uro alisema mradi huo wa Taka Sifuri mashuleni (Waste Zero School) una lengo la kutunza mazingira kwa kuondoa taka kwenye maeneo ya shule katika mkoa wa Dar es Salam ili kuhakikisha usalama wa kiafya kwa watoto wakiwa shuleni.


“Lengo ni kuhakikisha watoto wanasoma kwenye mazingira mazuri ili waweze kuelewa kile wanachojifunza, hivyo mradi huu utajikita kwenye utunzaji wa mazingira katika maeneo yao ili kuyafanya yawe sehemu salama wakati wakipata elimu,” alisema Mang’uro.


Mung’uro alisema watahakikisha taka zinapungua kwa asilimia 80 kwenye maeneo ya shule katika manispaa nne za jiji la Dar es salaam ambazo ni Dar es Salaam Jiji, Kinondoni, Kigamboni na Temeke.


Alitaja shule hizo za msingi kzilizo kwenye mradi huo kuwa ni Buzza, Temeke, Mbweni, Nguva, Kigamboni na Pugu.



Aidha mratibu huyo aliomba ushirikiano wa hali na mali kutoka kwa Wadau mbalimbali wa masuala ya utunzaji  wa mazingira nchi ili waweze kufanikisha malengo ya utunzaji wa mazingira shuleni kwa lengo la kuhakikisha shule panakuwa sehemu salama kiafya.


“Tutoe wito kwa wadau mbalimbali wanaohusika na kuongeza thamani za takataka na kuongeza thamani ya elimu yetu hapa Tanzania waweze kushirikiana na Taasisi ya mazingira Plus Pamoja na wadau  wengi katika kuhakikisha shule zetu nchini zinakuwa ni sehemu salama zenye afya, safi na nzuri kwa Watoto kujifunza”


Akizungumza kwenye warsha hiyo iliyokuwatanisha walimu na wataalamu mbalimbali, Afisa Mazingira kutoka Manispaa ya Kinondoni alisema yeye ni mdau mkubwa wa mpango wa Taka Sifuri hivyo anabeba dhima kubwa ya kuhakikisha utunzaji wa mazingira unafanikiwa kwenye manispaa yake.

“Nina adhima ya kusambaza elimu ya utunzaji wa mazingira na zaidi kutumia taka kama fursa kwa maana zipo taka zinazoweza kutumika kwenye uzalishaji mfano mbolea” alisema Mjabuso.

Kwa upande wake Mwalimu Kavuli Mushi wa Shule ya Sekondari ya Buza alisema kwenye warsha hiyo amepata nafasi ya kujifunza kuhusu utunzaji wa mazingira na atakuwa balozi mzuri wa mpango huo kwenye shule yake.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI