Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro (katikati) akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Makamba ya Burundi Nahimana Hamjsi (kulia) ambao walikuwa mabingwa wa mashindano ya Ujirani mwema yaliyofanyika nchini Burundi (wa pili kushoto) ni Mwenyeji wa mashindano hayo Mkuu wa Burunga nchini Burundi, Partfait Mboninyibuka na (kushoto) ni Mkuu wa mkoa Muhunga nchini Burundi, Denise Ndaruhekere wakishuhudia
Na Fadhili Abdallha,
Burunga Burundi
TIMU ya Kombaini ya wilaya Makamba mkoa Burunga nchini Burundi imetawazwa kuwa mabingwa wa mashindano ya ujirani mwema kwa mwaka 2025 baada ya kuifunga kombaini ya wilaya Kigoma kwa penati 4-2.
Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa michezo wa Nkurunzinza Peace Park Complex mkoa Burunga nchini Burundi timu hizo zilimaliza dakika 90 zikiwa hazijafunga katika mchezo ambao timu zote zilionyesha dhamiraa ya kubeba kombe la mashindano hayo.
Penati za timu ya Makamba ya Burundi yalifungwa na Ndayikengerukie Raymond, Ntakirutimana Fernand, Irakoze Emanuel na Nkurunzinza Pierre wakati yale ya Kigoma yalifungwa na Baraka Charles na Kassim Daud ambapo pambano hilo lilichezeshwa na Mwamuzi Emanuel Sonda wa Tanzania na washika vibendera walitoka Burundi.
Kwa matokeo hayo mabingwa hao wa mashindano hayo ya Ujirani mwema ameondoka na kitita cha fedha taslimu Faranga milioni saba sawa na shilingi milioni 2.5 za Tanzania wakati mshindi wa pili ambayo ni Kombainu ya wilaya ya Kigoma iliondoka ni kitita cha Faranga milioni tano sawa na milioni mbili za Tanzania.
Mshauri wa Mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wa masuala ya mafao, utawala, fedha, mipango, takwimu na diplomasia ya Maziwa Makuu, Esperance Muhindo (wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya fedha taslim kwa Nahonda wa Kombainu ya wilaya ya Kigoma Rashidi Malapa (kulia) ambao walikuwa washindi wa pili wa mashindano ya ujirani yaliyofanyika nchini Burundi (kushoto) Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon SirroMashindano hayo ambayo kwa mwaka huu yanakuwa yamefanyika kwa mara ya tisa mfululizo yalishirikisha jumla ya timu nane ambapo timu nne zinatoka mkoa Kigoma Tanzania na timu nne zinatoka mikoa ya Burundi na yaliendeshwa kwa njia ya mtoano.
Fainali ya Mashindano hayo yalihudhuriwa na Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro, Mwenyeji wa mashindano hayo Mkuu wa Burunga nchini Burundi, Partfait Mboninyibuka, Mkuu wa mkoa Muhunga nchini Burundi, Denise Ndaruhekere, Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Tanzania, Yussuph Singo.
Wengine ni Mshauri wa Mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wa masuala ya mafao, utawala, fedha, mipango, takwimu na diplomasia ya Maziwa Makuu, Esperance Muhindo pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa serikali za mitaa na wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama nchini Tanzania.
Wachezaji wa timu ya Kombaini ya Makamba mkoa Burunga nchini Burundi wakisherehekea ubingwa wa mashindano ya ujirani mwema baada ya kuifunga kombaini ya wilaya ya Kigoma kwa penati 4-2












0 Comments