Header Ads Widget

MADIWANI MBEYA DC WAPEWA MAFUNZO KATIKA UTUMISHI WAO.

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya wametakiwa kutambua wajibu wao na kuzingatia maadili ya utumishi kwa wananchi ili kufikia maendeleo endelevu badala ya kuwa katika kundi la walalamikaji.

Rai hiyo imetolewa na mkufunzi wa mafunzo kutoka Chuo cha Serikali za mitaa TAMISEEMI (Hombolo) Beyond Samweli Madege, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa mafunzo elekezi kwa waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya.

Mkufunzi huyo anasema madiwani wanapaswa kuzingatia sifa bora za uongozi ikiwa ni pamoja na kuwa na maono, kuzingatia maadili, kutunza siri na kushirikisha wananchi na viongozi wenzao ili kuleta ufanidi katika kazi.


Amesema katika baadhi ya maeneo kumekuwepo baadhi ya viongozi kuanzia ngazi za Serikali za mitaa ambao wamekuwa walalamishi badala ya kuwa sehemu ya utatuzi na ufumbuzi wa kero za wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Mhe. Aida Haule, amewataka madiwani wenzake kuzingatia elimu waliyopewa kwa ajili ya kuboresha utumishi wao wa kazi kwa manufaa ya wananchi wanaowahudumia.

Mhe. Aida ameishukuru kupitia Halmashauri yake (Mkurugenzi wa Halmashauri Halmashauri na watendaji) kwa kuruhusu chuo cha utumishi wa umma Tanzania TAMISEEMI Hombolo mkoani Dodoma kwenda kutoa mafunzo hayo muhimu kwa waheshimiwa madiwani wa jimbo la Mbeya vijijini.

Nao madiwani wa Halmashauri hiyo, wamesema mafunzo hayo ni muhimu na yanakwenda kuongeza ari kwenye utumishi wao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI