Header Ads Widget

KIBONDO,UVINZA ZATOLEWA MASHINDANO YA UJIRANI MWEMA

 

Mkuu wa mkoa Burungu Parfait Mboninyibuka (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa michezo mkoa Kugoma na Kombaini ya Wachezaji wamanispaa ya Kigoma Ujiji katika mashindano ya ujirani mwema nchini Burundi

Na Fadhili Abdallah,

Burungu, Burundi

 TIMU za wachezaji mchanganyiko za wilaya za Kibondo  na Uvinza za mkoani Kigoma nchini Tanzania zimeyaaga mashindano ya ujirani mwema yanayofanyika wilaya ya  Makamba mkoa Burungu nchini ambapo timu nne za Tanzania na nne za Burundi zinashiriki mashondano hayo yanayoendeshwa kwa njia ya mtoano.

                 Kombaini ya wachezaji wa wilaya ya Buhigwe mkoa Kigoma nchini Tanzania

Uvinza imeyaaga mashindano hayo kwa kufungwa goli 2-0 na wenyeji wa mashindano hayo Timu ya wilaya Makamba mkoa Burungu katika mashindano yanayofanyika kwenye uwanja wa Nkurunzinza Peace Park Complex ambapo timu ya Kibondo ilitolewa na Kombaini ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kufungwa goli 1-0.

                          Timu ya kombaini ya wilaya ya Makamba nchini Burundi

Awali timu ya Kombaini ya wilaya Buhigwe ya Tanzania ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuyaaga mashindano hayo baada ya kufungwa na timu ya  Muyinga ya nchini  Burundi baada ya kutandikwa mabao 2-1 ambapo hata hivyo na timu ya mkoa Muyinga ya nchini Burundi ilitolewa mashindano kwa kukiuka kanuni za mashindano.

Wachezaji wa kombaini za mkoa Muyinga nchini Burundi wenye jezi za Bluu Bahari na wachezaji wa kombaini ya wilaya Buhigwe mkoa Kigoma nchini Tanzania wakichuana katika mashindano ya ujirani mwema yanayofanyika wilaya ya Makamba mkoa Burungu nchini Burundi


Mjumbe wa kamati ya mashindano hayo Wilfred Lutera amethibitisha kuwa timu ya Muyinga ya nchini Burundi iliondolewa mashindano kwa kucheza Zaidi ya wachezaji 10 wenye umri wa Zaidi ya miaka 21 wakati kanuni inataka wachezaji wote wawe chini ya miaka 20 hivyo Buhigwe kupata nafasi ya kuendelea na mashindano.

MKUU wa mkoa Burungu nchini Burundi Parfait Mboninyibuka (kulia) akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa mashindano ya ujirani mwema Maarufu kama Lake Tanganyika Cup baina ya timu za Kombaini za wilaya za mkoa Kigoma na Kombaini za mikoa ya Burundi (kushoto) Wilfred Lutera mjumbe wa Kamati ya mashindano kutoka ofisi ya Mkuu mkoa Kigoma.


Katika mchezo mwingine timu ya Kombaini ya wilaya ya Nyanza ilitolewa kwenye mashindano hayo kwa kufungwa goli 2-1 na kombaini ya wilaya Ruyigi hivyo lufanya timu za Tanzania mbili na Burundi kuendelea na mashindano hayo ambapo Nusu fainali itafanyika siku ya jumatano.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI