Header Ads Widget

DEREVA RAIA WA RWANDA AKAMATWA AKIENDESHA LORI AKIWA MLEVI – POLISI WATOA ONYO KALI KWA NADEREVA.


Matukio Daima, Morogoro

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limemkamata na kumzuia kuendelea na safari dereva wa lori la mizigo, Uwimpue Bonheur (33), raia wa Rwanda, anayetokea nchini Kigali,baada ya kubainika akiendesha chombo hicho akiwa katika hali ya ulevi wa kiwango cha juu hatari kwa matumizi ya barabara.

Tukio hilo limetokea Desemba 27, 2025 katika eneo la Kihonda Kwachambo, Manispaa ya Morogoro, katika barabara kuu ya Morogoro–Dodoma, ambapo dereva huyo alikuwa akitokea Kigali kuelekea Dar es Salaam akiendesha lori lenye namba RAI 878 G, aina ya HOWO.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, kipimo cha ulevi kilionesha dereva huyo alikuwa na kiwango cha 171.7mg/100ml, kiwango kinachozidi kikomo kinachokubalika kisheria na kutishia usalama wa watumiaji wa barabara.

Aidha, Kamanda Mkama amesema hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya dereva huyo, huku akisisitiza kuwa jeshi la polisi halitavumilia watumiaji wa barabara wanaoendesha wakiwa wamelewa

Ametoa onyo kali kwa madereva wote kuacha tabia ya kuendesha wakiwa chini ya ulevi, akibainisha kuwa kitendo hicho kimekuwa chanzo cha ajali nyingi zinazosababisha vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI