KUFUATIA ripoti mbalimbali zilizotolewa na vyombo vya habari na mashuhuda, vurugu zilizotokea tarehe 29 Oktoba zimeleta uharibifu mkubwa wa miundombinu na mali binafsi katika miji kadhaa nchini, hususan katika Jiji la kibiashara la Dar es Salaam, pamoja na Mwanza, Arusha na Songwe na Iringa
Uharibifu huo umesababisha hasara kubwa ya mabilioni ya fesha kwa Taasisi na mashirika ya Umma, Watu binafasi na hata Taifa ujumla.
Taarifa zinaeleza kuwa vituo vya polisi vituo vya mabasi ya mwendokasi (BRT), pamoja na magari ya biashara na binafsi, vimeharibiwa, vingine vikiteketezwa kwa moto.
Aidha, miundombinu ya barabara imeathirika, ambapo baadhi ya barabara zilofungwa jambo lililosababisha usumbufu mkubwa katika usafiri wa watu na bidhaa.
Biashara nyingi katika miji mikubwa ziliripotiwa kuathirika, baadhi zikiporwa na kuharibiwa, huku majengo ya biashara,majengo ya ofisi za CCM, maduka, ofisi na nyumba za raia yakipata madhara kutokana na moto na mawe yaliyotumika wakati wa vurugu hizo.
Hata hivyo bado mamlaka za Serikali zinaendelea na tathmini ya kiwango cha uharibifu Katika maeneo yote yaliyoathirika.
Matukio Daima Media inatoa pole nyingi kwa wote walioathirika na vurugu hizi.






0 Comments