Header Ads Widget

UTABIRI WA TMA WATIMIA ,MVUA KUBWA YANYESHA IRINGA LEO

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

Mvua hii imenyesha ikiwa ni siku mbili toka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kutangaza matarajio ya uwepo wa hali mbaya ya hewa kwa siku tano kuanzia Jumatano Novemba 19, hadi Jumamosi Novemba 22, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka hiyo limetolewa angalizo la mvua kubwa ifikapo Alhamisi kwa maeneo machache ya mikoa ya Ruvuma na Njombe. 

Taarifa hiyo ilisema uwezekano wa kutokea kwa mvua hizo pamoja na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani. 


“Athari zinazoweza kujitokeza ni kuwa baadhi ya makazi kuzungukwa na maji. Zingatia na jiandae,” ilisema taarifa hiyo 


Maeneo machache ya mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Morogoro, Singida, Dodoma, Kigoma, Katavi na Tabora. 


“Uwezekano wa kutokea pamoja na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani,” imesema taarifa hiyo huku ikiongeza athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji. 

Aidha, ifikapo Jumamosi TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo ya mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Morogoro, Singida na Dodoma. 

“Uwezekano wa kutokea na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani. Athari zinazoweza kujitokeza: Baadhi ya makazi kuzungukwa na maji,” imesema taarifa hiyo. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI