Na Matukio Daima Media
MKAZI wa Mtaa wa Sangara, Chanika Mkoani Dar Es Salaam Bi. Aisha Athuman Yunga amesema hakuwahi kuzoea kile ambacho Kilitokea Oktoba 29, 2025, akimuomba Mwenyenzi Mungu kusaidia katika kuilinda na kuistawisha amani ya Tanzania.
Bi. Aisha pia ametoa wito kwa wananchi kuilinda amani na kutoshawishiwa kufanya tena vurugu na ghasia kama zilizotokea Jumatano ya Oktoba 29, 2025, akisema kutetereka kwa amani ya Tanzania ni kuharibika kwa maisha ya watanzania, hivyo ni muhimu kuilinda kwa maslahi ya Tanzania na ustawi wao binafsi.
"Tulishazoea kuwa uchaguzi ukifanyika, ukimalizika tunaendelea na shughuli zetu lakini siku ile ilikuwa siku ya tofauti kabisa na matokeo yake tukawekwa ndani suala ambalo hatuliwezi kutokana na mtindo wetu wa maisha, mimi niombe tu kila mtu aendelee kuhamasisha amani nchini." Amesema Bi. Yunga.
Bi Yunga pia amewashukuru Viongozi wa dini kwa kuendelea kuiombea Tanzania izidi kuwa na amani, akiwakumbusha wananchi kuwa amani ndiyo kila kitu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, akiwataka wananchi kuwakataa kwa nguvu zote wale wote wanaohamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, akiwataka Vijana kuachana na wanaofuata mikumbo na ushawishishi.








0 Comments