Header Ads Widget

RAIS MWINYI ATANGAZA MAWAZIRI WATEULE WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR


NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Mawaziri wateule, hatua inayolenga kuimarisha kasi ya maendeleo katika kipindi cha pili cha Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza leo, tarehe 13 Novemba 2025, Ikulu Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali katika awamu hii itakuwa na wizara 20 badala ya 18 zilizokuwepo awali, ili kuongeza ufanisi wa utendaji Serikalini.

Katika uteuzi huo, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza weledi, uadilifu na uzingatiaji wa maslahi mapana ya Taifa, sambamba na kutoa huduma kwa wananchi kwa uwazi na ufanisi.

Ameeleza kuwa uteuzi huo umezingatia uwiano wa kijinsia, uwakilishi wa Unguja na Pemba, pamoja na uzoefu wa viongozi katika sekta zao husika.

Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi  amesema kuwa nafasi za Wizara nne zikiwemo Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Afya, Utalii na Mambo ya Kale, pamoja na Biashara na Maendeleo ya Viwanda , zitaachwa wazi kwa muda hadi Serikali ikamilishe makubaliano na Chama cha ACT Wazalendo katika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Akitangaza Mawaziri na Naibu Mawaziri hao wateule, Dkt. Mwinyi ameyataja majina yao pamoja na Wizara watakazoongoza kama ifuatavyo:

MAWAZIRI

1. DKT. HAROUN ALI SULEIMAN, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora

2. MHE. DKT. SAADA MKUYA SALUM, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu

3. MHE. DKT. JUMA MALIK AKIL, Waziri wa Fedha na Mipango

4. MHE. IDRISSA KITWANA MUSTAFA, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, 

Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ

5. MHE. SHARIFF ALI SHARIFF, Waziri wa Kazi na Uwekezaji

6. MHE. HAMZA HASSAN JUMA, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi

7. MHE. RAHMA KASSIM ALI, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi

8. MHE. LELA MUHAMED MUSSA, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali

9. MHE. SHAABAN ALI OTHMAN, Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji

10. MHE. SULEIMAN MASOUD MAKAME, Waziri wa Kilimo,  Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo

11. MHE. NADIR ABDULLATIF ALWARDY, Waziri wa Maji, Nishati na Madini

12. MHE. MASOUD ALI MOHAMED, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi

13. MHE. DKT. KHALID SALUM MOHAMED, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

14. MHE. ANNA ATHANAS PAUL, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

15. MHE. MUDRIK RAMADHAN SORAGA, Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu

16. MHE. RIZIKI PEMBE JUMA, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

MANAIBU MAWAZIRI

1. MHE. BADRIA ATAI MASOUD, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

2. MHE. DKT. HAMAD OMAR BAKARI, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango

3. MHE. ALI ABDULGULLAM HUSSEIN, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo 

4. MHE. ZAWADI AMOUR NASSOR, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

5. MHE. SALHA MOHAMED MWINJUMA, Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi

6. MHE. SEIF KOMBO PANDU, Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini

7. MHE.DKT.SALUM SOUD HAMID, Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo

8. MHE. MBOJA RAMADHAN MSHENGA, Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi

9. MHE. MOHAMED SIJAMINI MOHAMED, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu

10. MHE. HASSAN KHAMIS HAFIDH, Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji

11. MHE. KHADIJA SALUM ALI, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI