NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kimedai kuwa wafanyakazi wake walivamiwa usiku wa kuamkia leo walipokuwa wakiendelea na kazi zao katika hoteli ya Whitesands iliyopo jijini Dar es Salaam, hali iliyozua taharuki kubwa na kuashiria hali ya wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wao.
Taarifa fupi iliyotolewa na kituo hicho kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, imedai kwamba hoteli nzima ilikuwa chini ya mashambulizi, huku timu ya LHRC ikiwa ndiyo lengo pekee. Vifaa vya kazi ikiwemo kompyuta na simu zao zilikamatwa na waliowavamia.
LHRC wamedai kuwa asubuhi ya leo, wafanyakazi hao wameitishwa kuhusiana na vifaa vilivyokamatwa, jambo ambalo limeongeza hofu kuhusu uhuru wao na uhuru wa taasisi za haki za binadamu.
Hata hivyo LHRC haijaweka bayana ni akina nani waliowavamia wafanyakazi hao, jambo ambalo limeacha maswali yasiyo na majibu
Taarifa zaidi zitakujia hapo baadae






0 Comments