Header Ads Widget

POLISI YAANIKA ORODHA HII YA VIONGOZI WANAOTAFUTWA KWA TUHUMA ZA KUCHOCHEA FUJO



Jeshi la Polisi Nchini limesema kufuatia uchunguzi na ushahidi uliokusanywa hadi sasa kuhusu vurugu zilizotokea October 29,2025, linawasaka kwa ajili ya kuwakamata Askofu Josephati Gwajima, Brenda Jonas Rupia, John Mnyika, Godbless Lema, Machumu Maximillian Kadutu (Askofu Mwanamapinduzi), Deogratius Mahinyila, Boniface Jacob, Hilda Newton, Award Kalonga na Amaan Golugwa.


Taarifa iliyotolewa usiku wa Novemba 7 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini imesema Jeshi la Polisi linawataka Watu hao kujisalimisha katika Vituo vya Polisi mara moja watakapoona taarifa hii popote pale walipo.



"Pamoja na kwamba baadhi ya waliopanga na kutekekeza uhalifu huo wamekamatwa na kuanza kufikishwa Mahakamani, Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta wale wote waliopanga, kuratibu na kutekeleza uovu huo, wakati hatua hizo zikiendelea Jamii inaombwa kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kutoa taarifa za Watu wote waliohusika ili hatua sahihi za kisheria zichukuliwe dhidi yao" taarifa hiyo.</

p>

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI