Header Ads Widget

DKT TULIA AJIONDOA KUGOMBEA USPIKA

 



Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Tulia Ackson, ametangaza kujiondoa rasmi katika kugombea nafasi hiyo leo, Novemba 7, 2025.


Dkt. Tulia, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, na kwa sasa ni Mbunge mteule wa Jimbo la Uyole, ametoa tangazo hilo bila kubainisha sababu za kujiondoa kwake hadi sasa.


Dkt. Tulia Ackson aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alichaguliwa kuwa Spika tarehe 1 Februari 2022, baada ya kuchaguliwa na wabunge wa Bunge hilo, kuchukua nafasi iliyokuwa wazi wakati huo.


Aidha, kwa sasa anahudumu pia kama Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI