Header Ads Widget

NIMEUNDA TUME KUCHUNGUZA CHANZO, VURUGU ZA OKTOBA 29- RAIS SAMIA


Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza Wabunge wa Bunge la Tanzania na wageni waalikwa kusimama na kuomba kwa dakika moja kwaajili ya Wananchi waliopoteza maisha kwenye vurugu na ghasia za Jumatano ya Oktoba 29, 2025 katika Miji ya Arusha, Dar Es Salaam, Mbeya, Mwanza na Songwe.

Rais Samia ameongoza jambo hilo leo Ijumaa Novemba 14, 2025 Bungeni Mjini Dodoma wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la 13 la Tanzania akitangaza pia kuunda Tume maalumu ya kuchunguza tukio hilo, akitoa pole pia kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao.

"Serikali imechukua hatua ya kuunda Tume ya kuchunguza yaliyotokea ili tujue kiini cha tatizo, taarifa hiyo itatuongoza kujielekeza kwenye mazungumzo ya kuleta maelewano na amani." Ametangaza Rais Samia.

Akieleza namna ambavyo ameumizwa na tukio hilo, Rais Samia pia amewaombea kheri majeruhi wote huku pia akiwaomba waliopoteza mali zao kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI