Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amempongeza na kumshukuru Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa mchango aliyoutoa wakati wa kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha kwanza cha Awamu ya Sita.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Makamu wa Rais, yaliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. Amesema kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha kwanza cha Awamu ya Sita, ambayo ilitoa urahisi wakati wa ufanyaji kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Makamu wa Rais amesema ataendeleza jukumu la kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwezo wake wote ili kutekeleza vema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wake Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Philip Mpango amempongeza Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa nafasi hiyo muhimu na kumsihi kutekeleza vema majukumu ya kuwa mshauri namba moja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemsihi kutumia hekima na unyenyekevu wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Novemba 04, 2025
Ikulu - Chamwino.






0 Comments