Header Ads Widget

MWANDISHI WA HABARI AFARIKI DUNIA


Na Matukio Daima Media, Mbeya

ALIYEKUWA  mtangazaji wa Bomba FM Mbeya, na kwa sasa akihudumu kama dereva wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Azza Kamendu (39), amefariki dunia leo katika ajali mbaya ya uso kwa uso iliyotokea saa 1:00 asubuhi, Novemba 14, 2025, katika eneo la Senjele, Wilaya ya Mbozi, barabara kuu ya Tunduma-Mbeya, mkoani Songwe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Agustino Senga, amethibitisha kuwa ajali hiyo ilihusisha Lori la FAW lenye namba T.717DWD/T.847DQT mali ya Midwest Minerals Ltd, lililokuwa likitoka Tunduma kwenda Mbeya, na Toyota Land Cruiser namba SU.43390 mali ya NIMR.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali ni "wrong overtaking", ambapo dereva wa lori la FAW alijaribu kupita magari mengine katika eneo hatarishi bila uangalifu, na kusababisha mgongano wa uso kwa uso na gari la NIMR. Azza Kamendu alifariki dunia papo hapo, huku magari yote yakiwa yameharibika vibaya.

Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali kumtafuta dereva wa lori hilo, ambaye alikimbia mara baada ya ajali na bado hajapatikana. Kamanda Senga ametoa wito kwa madereva wote kuzingatia sheria, alama na michoro ya barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

Azza Kamendu atakumbukwa kama mtangazaji mahiri wa vipindi vya Injili kupitia Bomba FM, alikopata heshima na upendo kutoka kwa wasikilizaji wa Mbeya na nje ya mkoa.

Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI