Header Ads Widget

MBUNGE MTEULE AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA

 


Mahakama ya Wilaya ya Kiyumba nchini Rwanda imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela Germain Musonera kwa kuhusika na mauaji ya halaiki na kumtaka kulipa fidia ya faranga milioni 50 kwa shirika la walionusurika IBUKA.

Musonera alikana mashtaka dhidi yake katika kesi iliyosikilizwa katika wilaya ya Ndiza ya wilaya ya zamani ya Nyabikenke kwani huko ndiko uhalifu ulidaiwa kutendeka na alikozaliwa.

Upande wa mashtaka ulitaka afungwe maisha jela na kulipa fidia ya milioni 500 kwa walionusurika.

Kesi ya Musonera imejadiliwa sana kwa sababu mwanachama huyo wa chama tawala cha RPF-Inkotanyi alikamatwa baada ya uchaguzi wa mwaka jana akiwa kwenye orodha ya kuingia bunge la Rwanda kama mbunge wa chama hicho.

Siku moja kabla ya kuapishwa miongoni mwa wabunge wengine waliochaguliwa, chama chake kilimuondoa kwenye orodha hiyo na akatupwa nje.

Kabla ya kufungwa alikuwa mkurugenzi katika ofisi ya waziri mkuu wa Rwanda.

Mahakamani, upande wa mashtaka ulisema Musonera alihudumu kama kiongozi wa vijana katika wilaya ya Nyabikenke wakati wa mauaji ya kimbari.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI