Baada ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutangaza baraza jipya la mawaziri huku baadhi ya mawaziri wa zamani wakiachwa akiwo aliyekuwa waziri wa Kilimo Hussein Bashe
Waziri huyo wa zamani ameandika ujumbe huu katika page yake ya Instagram .
SOMA Hapa chini👇👇👇👇
Bashehussein Salaam ndugu zangu,
Natumia nafasi hii kumshukuru Allah kwa kila jambo na kwa baraka zake katika safari yangu ya utumishi.
Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassa kwa imani kubwa aliyonionyesha katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi kama Naibu Waziri, na baadae kuniteua kama Waziri wa Kilimo.
Ni heshima niliyothamini kwa moyo wangu wote, na ninaendelea kuwa mwenye shukrani kwa nafasi hiyo ya kuwatumikia Watanzania.
Natoa pongezi za dhati kwa Ndugu Daniel Chongolo kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo. Namfahamu kama Mkulima na mzalendo. Nina uhakika atamsaidia Mheshimiwa Rais kutimiza matarajio ya Watanzania.
Vilevile, nampongeza Ndugu yangu David Silinde kwa kuendelea kuaminiwa kama Naibu Waziri. Sina mashaka nae Mzazi najua atakuwa msaada mkubwa kwa Waziri wake.
Nawashukuru pia watumishi wote wa Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano wa hali ya juu mlionipa katika kipindi cha miaka sita. Nawatakia heri na fanaka katika kuendelea kutekeleza majukumu yenu ya kuwatumikia Watanzania.
Asanteni sana.
Last Slide - turudi shambani
mariam_ditopile Wakulima hatutakusahau ...kila la heri kwenye utumishi wa wana Nzega







0 Comments