Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi Sudi Mwakibasi akitoa tamko kwa Wakimbizi wa Burundi wqnaohifadhiwa kwenye kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu wilaya ya Kasuku mkoani Kigoma la kufuta hadhi ya ukimbizi kwa wakinbizi hao
Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), Barbara Bentum Dotse (kushoto) akizungumza wakati wa zoezi la kutoa tamko za hatua ya kufuta hadhi ya ukimbizi kwa wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Serikali ya Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) wamekubaliana kwa kauli moja kufuta hadhi ya ukimbizi kwa wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa mkoani Kigoma na wakimbizi wote wanatakiwa kuondoka kwenye kambi hizo ifikapo juni 30 mwaka 2026.
Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Sudi Mwakibasi ametangaza hayo kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambapo alisema kuwa kwa sasa wakimbizi wa Burundi wanahofadhiwa kwenye kambi za Nyarugusu wilaya ya Kasulu na Nduta wilaya ya Kibondo hawana hadhi na sifa ya kuwa wakimbizi.
Mwakibasi alisema kuwa kabla ya kufikia hatua hiyo walifanya mahojiano ya wakimbizi wote kwa kila kaya kwa wakimbizi waliopo kambini na nje ya makambi mahojiano yaliyofanyika kuanzia mwezi Mei hadi Agosti mwaka huu ambapo imethibitika kuwa wakimbizi hao hawana sababu yeyote inayowafanya kuendelea kuwa na hadhi ya ukimbizi nchini.
Kufuatia hali hiyo Mkurugenzi huyo wa idara ya wakimbizi alisema kuwa wakimbizi hao wanapewa muda wa kujandikisha kwa hiari na kurudishwa nchini kwao kwa hairi zoezi litakalofanyika hadi mwezi juni mwaka 2026 na kwamba baada ya hapo itakuwa inabandikwa orodha ya wakimbizi wanaotakiwa kuondoka na watakaogoma watachukuliwa hatua kwa mujibu wa makubaliano ya pande tatu yaliyofanyika.
Kwa upande wake Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), Barbara Bentum Dotse alisemaa kuwa asilimia 90 ya wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa kwenye makambi ya Nyaarugusu na Nduta mkoani Kigoma hawana hadhi yaa kuendelea kuwa wakimbizi na uamuzi pekee dhidi yao ni kurejea nchini mwao.
Mwakilishi huyo alisema kuwa sababu kubwa ambayo imegundulika wakaati wa mahojiano inaonyesha wakimbizi wengi wana chaangamoto ya kutokuwa na mashamba, ajira na masuala ya kiuchumi mambo ambayo yanaweza kushughulikiwa wakiwa nchini kwao na siyo kwenye makambi wakiishi kama wakimbizi.
Naye Balozi Mdogo wa Burundi katika ubalozi wa Kigoma nchini, Kekenwa Jeremia alisema kuwa amekuwa akishughulikia changamoto mbalimbali za wakimbizi hao lakini hakuna changamoto ya kuwafanya waendelee kuwa wakimbizi na nyumbani nchini Burundi Amani ipo ya kutosha hivyo wakimbizi hao wanapaswa kurejea nchini mwao.
Mwisho.
0 Comments