Vingozi mbalimbali duniani wameendeela kutuma risala zao za rambirambi kufuatia kifo cha Jane Goodall, mwanasayansi aliyegundua ukaribu wa sokwe na binadamu.
Rais wa Tanzania, ambako Goodall alisomea sokwe, amasema "kazi yake ya Hifadhi ya Kitaifa ya Gombe ilibadilisha uhifadhi wa wanyamapori."
Utafiti huo "uliweka nchi yetu katika kiini cha juhudi za kimataifa za kulinda sokwe na asili," Rais Samia Suluhu aliandika kwenye X.
Mwanmfalme Harry na mkewe Meghan walimsifu Goodall kama "mwanasayansi mwenye maono ya kibinadamu, mwanasayansi, rafiki wa sayari na rafiki yetu."
"Ahadi yake ya kubadilisha maisha inaenea zaidi ya yale ulimwengu uliona, na pia kwa yale ambayo sisi binafsi tulihisi."
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guttierez, alinukuliwa akisema katika X: Goodall anaacha "urithi wa ajabu kwa ubinadamu na sayari yetu," "Nimesikitishwa sana kuhusu kifo cha Jane Goodall, Mjumbe wetu mpendwa wa Amani," aliongeza, akirejelea nafasi ya heshima aliyoipata Goodall tangu 2002 katika shirika la kimataifa kwa kazi yake ya uhifadhi.
"Zaidi ya yote, Jane alitufundisha kwamba tunapotafuta ubinadamu katika ulimwengu wa asili unaotuzunguka, tunagundua ndani yetu wenyewe," rais wa zamani wa Marekani Joe Biden alisema.
Mnamo Januari, katika siku za mwisho za uongozi wake, Biden alimtunukia Goodall Nishani ya Rais ya Uhuru -- heshima ya juu zaidi ya kiraia katika taifa hilo.






0 Comments