Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA,Mkoani Kagera wamefungua juma (week) ya Huduma Kwa wateja Kwa kuwatembelea na kutatua changamoto za Wafanya biashara.
Akizungumza baada ya kuwatembelea Wafanya biashara hasa walipa Kodi,Naibu kamishina Wa Upelelezi Wa Kodi Tanzania Ndg,Hashimu Ngoda,amesema lengo la kufanya hivo ni kuwasikiliza na kujua ni namna Gani wanahudumiwa na mamlaka hiyo Kwa Nia ya kutatua changamoto na kuboresha zaidi.
" Haya yote ni maelekezoa ya Kamishina Mkuu kwamba tupite Kwenye Maeneo yote ya Wafanya biashara tuzungumze nao na tuwasililize ili tuweze kujua changamoto zao na namna tunavyowahudumia na pengine tupokee ushauri kutoka kwao ili tuboreshe zaidi huduma zetu,amesema Ngoda"
Ngoda,amesema kuwa Kila mfanya biashara ana haki ya Kupata huduma Bora kutoka kwenye mamlaka hiyo na kusema kuwa Katika juma (week) ya Huduma Kwa wateja Kila mfanya biashara mlipa Kodi atatembelewa bila kubagua analipa Kodi kiasi Gani.
Amewasisitiza wafanya biashara kutoa risiti pindi wanapouza na kununua bidhaa pamoja na wanunuzi kudai risiti pamoja na kutumia machine za EFD kwani kufanya hivo ni wajibu Wao Wa kizalendo Wa kusaidia ukusanyaji Wa mapato.
Nao baadhi ya Wafanya biashara waliotembelewa Katika ofisi zao akiwemo Bi, Husna Mohamed na Kisha Ilamulila Mkuu Wa Shule za Kemebos na Kaizirege ,wamewasihi Wafanya biashara wengine kujitokeza kulipi kodi huku wakisema kufanya hivo ni kuchangia Katika maendeleo ya jamii na nchi Kwa ujumla.
0 Comments