Header Ads Widget

SIRRO ATAKA WAZAZI KUHIMIZA MASOMO YA SAYANSI KWA WATOTO WAO


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka  wazazi mkoani Kigoma kuhamasisha watoto wao kuyapenda  masomo ya Sayansi ili taifa liweze kuzalisha idadi kubwa ya wataalam ambao  watalitumikia taifa kupitia Sekta  zinazotokana na masomo ya sayansi.

Balozi Sirro ametoa amesema hayo akikagua  ujenzi wa Maabara tatu za  masomo ya Kemia, Baiolojia na Fizikia katika Shule ya Sekondari ya  Kakonko mkoani Kigomau ukiwa ni moja ya miradi inayotekelezwa  na Shirika la Umoja  wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF)  kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) kwa gharama ya Shilingi Milioni 180.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa serikali imekuwa ikihimiza wanafunzi kusoma masomo ya sayansi na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wanaofanya vizuri ili kusaidia kuongeza morali ya kuinua wanafunzi kusoma masomo ya sayansi na kupata idadi kubwa ya wataalam wanaotokana na kozi mbalimbali zinazotokana na masomo ya sayansi.


Kutokana na hali hiyo Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa wazazi wanalo  ni jukumu la kubwa la kuwahimiza na kuwaandaa watoto wao kusoma masomo yao sayansi sambamba na kuwasaidia katika kuwawekea mazingira mazuri ambayo watoto watasoma masomo hayo na kuyapenda.

Akizungumzia ujenzi wa maabara hizo Mkuu huyo wa mkoa Kigoma amewataka wanafunzi, wazazi na jumuia nzima ya shule hiyo kuilinda na kuitunza miundombinu hiyo  muhimu ya kujifunzia na kufundishia  ili iweze kutumika kwa muda mrefu na kunufaisha kundi kubwa la watanzania.

Awali Mkuu wa Shule hiyo, Anatoria Paul alisema  kuwa kukamilika kwa mradi huo kumeongeza hamasa kwa wanafunzi wengi kusoma masomo ya Sayansi sambamba na kufanya vizuri katika masomo hayo kutokana na kuwepo kwa vifaa kutosha vya kujifunzia na kufundishia.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI