Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha ameongoza maelfu ya Wananchi Mkoani humo kufanya Matembezi Maalumu kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Mkuu huyo wa Mkoa akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga wameongoza Wananchi hao katika matembezi na mazoezi mbalimbali yaliyofanyika katika Barabara za Mitaa mjini Bariadi.
Macha amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura pia kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha amani siku ya uchaguzi.
"Tujitokeze kwa wingi kupiga kura, ili kupata viongozi wanaotufaa, pia tushirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha amani siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi" amesema.
Mwisho.












0 Comments