NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
IRINGA.Mgombea Ubunge Jimbo la Iringa Mjini Fadhili Ngajilo amesema atahakikisha kata Ruaha inarejea katika viwanda vya kimkakati ili kuinua uchumi wa wananchi mmoja mmoja.
Ngajilo amesema hayo leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Ruaha na kubainisha kuwa kata hiyo iliwahi kuwa na viwanda vingi ambavyo kwa sasa havipo.
Alisema kuwa ukuaji wa uchumi wa Iringa unategemea na ukuaji wa viwanda vikubwa, vya kati pamoja na viwanda vidogo vidogo .
"Ilani ya uchaguzi imetamka kuwa kuna viwanda vya kimkakati vitajengwa iringa, viwanda vikubwa vya kati na vidogo vidogo, na Ilani hiyo imesisitiza kibwabwa na Nduli zinaenda kuanzishwa kongani za viwanda ili kusaidia ukuaji wa uchumi na ajira kwa wananchi wa Iringa"
Aliongeza kuwa Atahakikisha anazungumza na wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa ili waweze kwenda Iringa kuwekeza na kujenga viwanda.
Akizungumzia suala la wakulima alisema kuwa lengo kubwa ni kuwawezesha katika kuwapa elimu ya ujasiliamali na kuwapa mikopo yenye riba nafuu ili waweze kuendesha kilimo chenye tija.
Aidha alisema kuwa atawatoa wakulima katika kilimo cha chakula na kuwapeleka katika kilimo cha biashara na kuhakikisha wanapata masoko ndani na nje ya iringa.
"Nataka tutoke katika kilimo cha chakula yaani unalima ili ule chakula, nataka tutoke hapo na kwenda kwenye kilimo cha ujasiliamali,
Alisema kuwa Manispaa ya Iringa Asilimia 33 ya wakazi wa Iringa ni wajasiliamali na asilimia 31 ni wakulima
"Mimi kama mbunge ninawaahidi nitasimama na wakulima kutokana na changamoto zao hasa katika upande wa mbolea na katika ilani imetajwa na itaongezwa kutoka tani 21,000 kwenda tani 38,000 ya mbolea ya ruzuku"alisema
MWISHO.
1 Comments
Ushuhuda Wangu Wa Dhati 💖
ReplyDeleteBaada ya baba yangu mdogo kuniacha kwa miezi saba ndefu, nilivunjika kabisa. Alinifungia kwenye mitandao yote ya kijamii, akasafiri mbali, na hakukuwa na njia ya kumfikia. Nilikaribia kukata tamaa juu yetu, lakini ndani kabisa nilijua singeweza kupata mtu yeyote ambaye angenipenda na kunitendea jinsi alivyonitenda.
Siku moja, bosi wangu kazini aliona jinsi nilivyokuwa na huzuni na akanitambulisha kwa Dk. Dk. Dawn alisikiliza hadithi yangu na akaahidi kwamba mpenzi wangu atanirudia ndani ya siku tatu. Kusema kweli, sikuamini mwanzoni—lakini kwa mshangao mkubwa zaidi, siku ya tatu simu yangu iliita. Ilikuwa ni yeye! Alikuwa akilia na kuomba msamaha, akisema hataniacha tena.
Tangu siku hiyo, uhusiano wetu umekuwa wenye nguvu na mzuri zaidi kuliko hapo awali. Amekuwa akinipenda na kunijali sana mimi na mtoto wetu, na sasa tunafunga ndoa baada ya miezi miwili tu! ❤️
Shukrani zote kwa Dk. Dawn, ambaye kwa kweli aliwezesha jambo lisilowezekana. Ninampendekeza kwa moyo wote kwa yeyote anayekabiliwa na changamoto katika:
Masuala ya mahusiano au ndoa
Ugonjwa au magonjwa
Ugumba au matatizo ya bahati nasibu
Kesi za mahakama au kurejesha mali
Dk. Dawn kweli hutatua matatizo kwa ufanisi na hurejesha furaha katika maisha ya watu.
Wasiliana na Dr. Dawn kwenye WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com