Header Ads Widget

JWTZ NA POLISI MOROGORO WAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KUJIIMARISHA KATIKA ULINZI NA USALAMA

 

Majeshi ya Ulinzi na Usalama mkoani Morogoro  Oktoba 18, 2025, yamefanya mazoezi ya pamoja yenye lengo la kuimarisha mshikamano, ushirikiano na utayari wa kulinda usalama wa wananchi na mali zao.


Akizungumza wakati wa mazoezi hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema mazoezi hayo ni sehemu ya maandalizi ya kawaida na yanalenga kuongeza ufanisi wa vyombo vya ulinzi na usalama, siyo kuwatisha wananchi kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodhani.

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa jamii kuelewa kuwa kuwepo kwa mazoezi hayo ni ishara ya utayari wa vyombo hivyo katika kukabiliana na changamoto za kiusalama, hususan kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu.


Kwa upande wao, baadhi ya washiriki kutoka majeshi mengine wameeleza kuwa mazoezi hayo yanasaidia pia katika kuimarisha afya ya miili yao, kuleta mshikamano miongoni mwa vikosi mbalimbali na kujenga ushirikiano imara unaohitajika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI