Header Ads Widget

MSIGWA AKANUSHA KUHUSIKA NA SCREENSHOT ZA KUPOTOSHA INSTAGRAM


Na Matukio Daima Media

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amekanusha vikali taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa ame-like chapisho la mtandaoni lililotumwa na akaunti ya @mangekimambi80 katika mtandao wa Instagram.

Taarifa hizo zilienea kwa kasi mitandaoni zikiambatanishwa na screenshots zinazodaiwa kuonesha akaunti yake rasmi ikijihusisha na maudhui hayo, jambo ambalo Msigwa amelitaja kuwa ni uongo na upotoshaji unaolenga kuchafua taswira yake.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram @gersonmsigwa, Msigwa alitoa kauli kali ya kukemea kitendo hicho akikitaja kama uchochezi na ubabaishaji wa mitandaoni unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa.


Katika ujumbe wake, Msigwa aliandika:

"KUNA MWEHU MMOJA NA GENGE LA WEHU WENZAKE WANAHANGAIKA KUTENGENEZA SCREENSHOTS KWA PHOTOSHOP ZINAZOONESHA MIMI @GERSONMSIGWA NIME-LIKE UJINGA WAO WA KIPUUZI. YAANI WANAJITEKENYA ILI WACHEKE.

ACHENI UPUUZI. HII LEVEL NI TOFAUTI SANA. MICHEZO HII TULIICHEZA KITAMBO. WATANZANIA NI WATU WELEVU SANA HAMTAWAPATA KWA KUPIGA MAMBO KIJINGAJINGA NAMNA HII.

MSIJE TENA BILA GUARD HAKUNA KITONGA HAPA. NA BAHATI YENU NILISHAACHA USELA. BE TENDER GUYS."

Ujumbe huo wa Msigwa ni  kama onyo kwa watu wanaotumia teknolojia na mitandao ya kijamii kutengeneza taarifa za uongo (fake news) na kusambaza taswira potofu za viongozi na taasisi nchini.

Tukio hilo limeibua mjadala mpana kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na athari za kuzusha taarifa zisizo na uhakika. 

Ifahamike ni kosa kisheria kusambaza taarifa za uongo mitandaoni hivyo ni vema kila mmoja kuwa makini na kuepuka kuchapisha ama kusambaza taarifa za uogo .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI