Na Matukio Daima Media , Iringa
Kazi kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwashawishi viongozi wa vyama vya upinzani kuhamia CCM, wakiamini kuwa ndicho chama chenye dira ya ushindi na maendeleo nchini.
katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Kihesa, viongozi wanne wa chama cha CHAUMA kutoka mikoa ya Iringa na Njombe walitangaza rasmi kurejea CCM na kukabidhi kadi zao kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daud Yasin, wakati wa kilele cha kampeni za mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Iringa Mjini, Fadhili Ngajilo.
“Ahadi zinatekelezwa kwa vitendo” – Yasin
Akihutubia mamia ya wananchi waliofurika uwanjani hapo, Yasin alisema utekelezaji madhubuti wa Ilani ya Uchaguzi ya 2020/2025 ndiyo unaoifanya CCM kuaminiwa zaidi. “Desturi ya CCM ni moja tu: Tukiahidi — tunatekeleza.
Wananchi wa Iringa mna kila sababu ya kuwa na imani nasi,” alisema huku akishangiliwa.
Yasin alibainisha kuwa Ilani ya CCM 2025–2030 imeweka msisitizo zaidi katika kuongeza kasi ya maendeleo Jimboni Iringa, hususan katika sekta za afya, elimu na uchumi wa wananchi.
Miradi mikubwa ya maendeleo
Akieleza ahadi za chama kwa jimbo hilo, Yasin alisema ya Afya kwa Kujenga zahanati 2 mpya, vituo vya afya 3, na kuboresha miundombinu katika Hospitali ya Frelimo.
kwa upande wa Elimu Kujenga vyumba 294 vya madarasa, maabara 40, mabweni 8, mabwalo ya chakula 7, matundu ya vyoo 1,000, na kukarabati shule kongwe 2.
Biashara na uchumi
Ujenzi wa soko kubwa la kisasa Machinga Complex eneo la Stendi ya zamani, kukamilisha Stendi ya Igumbilo, ukarabati wa masoko 7, machinjio ya kisasa Ngelewala, ujenzi wa ofisi 40 za mitaa na kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa vikundi zaidi ya 500.
“Hii ndiyo CCM — kazi kwa vitendo, si maneno,” alisisitiza.
“Hakuna jipya CHAUMA” – Viongozi waliohamia CCM
Miongoni mwa viongozi waliojiunga na CCM ni Diana Benedikto – Mwenyekiti CHAUMA Mkoa wa Iringa na Mjumbe wa Sekretarieti ya Taifa
Ibrahim Idd – Katibu CHAUMA Mkoa wa Iringa
Makuke Mjinja – Mwenyekiti CHAUMA Mkoa wa Njombe
Diana Kivina – Katibu CHAUMA Mkoa wa Njombe
Benedikto alisema ameamua kurudi CCM kwa hiari akiamini ni chama chenye misingi ya amani na maendeleo.
“CHAUMA hakuna jipya. Huku CCM kuna kazi, amani na maendeleo,” alisema.
Kwa upande wake, Idd alisifu uadilifu na ukweli ndani ya CCM kama sababu ya kurejea.
“Tumefanya kampeni za kimkakati” – Rubeya
Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Iringa, Said Rubeya, alisema kampeni za mwaka huu zimeendeshwa kwa amani na ubunifu kubwa, zikifika kwa wananchi katika kila eneo.
“Hakuna nyumba tuliyoshindwa kufika. Wananchi wamempokea vizuri mgombea wetu,” alisema.
Ngajilo
Tutaboresha mikopo, michezo ipae
Mgombea ubunge wa CCM, Fadhili Ngajilo, aliwahakikishia wananchi programu madhubuti za kukuza uchumi na ujasiriamali kupitia mikopo inayotolewa kwa wakati, ikijumuisha vifaa vya kazi, si fedha pekee.
Katika michezo, aliahidi kufufua ushindani wa soka Iringa: “Kila kata itakuwa na timu bora. Tutaunda timu ya manispaa itakayopanda Ligi Kuu — Iringa inarudi kwenye ramani ya michezo.”
Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Jesca Msambatavangu, aliwataka wananchi kuendelea kuweka mbele maslahi ya taifa zaidi ya maslahi binafsi na vyama. 


















































0 Comments