Header Ads Widget

BODABODA NA MACHINGA HATUTAKUWA CHANZO KUVUNJA AMANI YETU

 

Na Matukio Daima Media

Makundi ya waendesha bodaboda na wamachinga yamezunguka katika mitaa kadhaa ya jiji la Dar es Salaam ikiwemo Posta, Kisutu, Kivukoni, Kariakoo, Karume, na Buguruni, yakihamasisha wananchi kulinda amani na kujitokeza kupiga kura siku ya tarehe 29 Oktoba.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kiongozi wa waendesha bodaboda Ilala, Abdul Kimaro, amewataka vijana wenzake kutokubali kurubuniwa kufanya vurugu na badala yake kutumia haki yao ya kidemokrasia kwa kupiga kura kwa amani.


Kwa upande wao, makundi ya bodaboda na wamachinga wameonesha kukubali elimu hiyo, huku baadhi yao wakiapa kujitokeza kupiga kura na kusisitiza kuwa hawatashiriki katika vurugu za aina yoyote.

Viongozi wengine wa wamachinga na wajasiriamali wadogo (mama na baba lishe) na bodaboda nao wamejitokeza kuunga mkono kampeni hiyo ya amani, wakisisitiza kuwa uchaguzi ni fursa ya maendeleo na siyo sababu ya migogoro.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI