NA NAMNYAKI KIVUYO, MATUKIO DAIMA ARUSHA.
Chama cha waandishi wa habari mkoa Arusha (APC)kwa kushirikiana na wataalamu wa afya pamoja na vikundi vya mazoezi(Jogging clubs) wamefanya usafi katika kituo cha afya Levolosi pamoja na Kaloleni kuelekea tamasha la michezo linalotarajiwa kufanyika Oktoba 18,2025 lenye lengo la kutokomeza magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba 29,2025.
Akiongea na waandishi wa habari katika zoezi hilo Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Arusha Claud Gwandu alisema kuwa kwa kushirikiana na wadau wameandaa tamasha la michezo litakalofanyika Oktoba 18,2025 ambapo tamasha hilo litahusisha michezo mbalimbali, upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza pamoja na ushauri.
"Wataalamu wa Afya wamekuwa wakituambia kuwa kinga kubwa ya magonjwa haya ni kufanya mazoezi kwa maana hiyo michezo na afya ni vitu vinavyohusiana na sisi kama waandishi tumepoteza wenzetu wengi kutokana na magonjwa haya hivyo tunafikiri tamasha hili litakuwa sehemu ya kutafuta tiba kwani kutakuwa pia na elimu ya afya.
"Tumeona tatizo linazidi kuwa kubwa na badala ya kuja kuangaika na tiba hapo baadae tuanze kuchukua hatua hivyo nimawaalika waandishi wenzangu hiyo tarehe 18 ambapo tutatangaza tunafanyia wapi ila kwa sasa maandalizi yanaendelea nia ikiwa ni tuwe na afya bora ili tuweze kufanya kazi zetu kwa ukamilifu." Alieleza
"Sisi tuna majukumu makubwa sana ya kuwaelimisha wananchi, kuwahamasisha hasa katika jukumu kubwa la kitaifa la uchaguzi oktoba 29 ambapo tunahitaji watu wajitokeze kupiga kura, kwahiyo kama tusipokuwa na afya njema tutakosa nafasi ya kuwahamasisha na kuwaelimisha,"Alisema
"Katika hili tunawaomba wananchi Oktoba 29 wajitokeze kwa wingi kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi watakao liongoza taifa kwa kipindi cha miaka mitano kwaajili ya maendeleo yetu,tunataka watu wakapige kura bila sasiwasi wowote na wachague kiongozi wanaemtaka latika ngazi ya udiwani,Ubunge na Urais," Alisisitiza.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt Charles Rashid alisema kuwa katika tamasha hilo kama wataalamu wa afya watatoa huduma ya uchunguzi wa magonjwa yasiyo ambukiza kwasababu michezo inapambana na kupunguza magonjwa kwa wananchi.
"Tutaweka wataalamu wa afya wa afya ya akili kwasababu sasa hivi kuna changamoto nyingi za afya ya akili kwa watu wa rika mbalimbali lakini pia tutakuwa na huduma za dharura wakati michezo ikiendelea ili kuhakikisha kwamba jambo hili mahususi kwa watu wa Arusha linaenda vizuri na linafana," Alisema Mganga mkuu.
Aidha aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuimarisha huduma za afya kwa mkoa wa Arusha ambapo pamoja na uboreshaji na ujenzi wa miundombinu kwasasa kituo cha afya wana mashine za ultra sound na xray za kidigitali ambazo zilikuwa zinapatikana kwenye hospitali za rufaa pekee hivyo Kupitia huduma hizo zilizoboresha aliwaomba wananchi kujiitokeze Oktoba 29 kupiga kura," Alisisitiza
Aisha mbwana mwanachama wa jogging club alisema kuwa mazoezi na afya ni kitu kimoja ambapo wameona ni vema kujitolea kufanya usafi kwenye vituo hivyo ili kuunga serikali mkono pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza Octoba 29, kupiga kura.
Maria Joseph mmoja wa wagonjwa waliokuwa wakipatiwa huduma ya mama na mtoto katika kituo cha Afya Levolosi alisema kuwa anaishukuru serikali kwani amepata huduma nzuri na kufanikiwa kujifungua mtoto wa kike ambapo aliwahamasisha wananchi kuishukuru
Serikali kwa kujitokeza kupiga kura.Yahaya Zuberi ambaye pia ni mwanachama wa jogging alieleza kuwa wanathamini mchango mkubwa uliofanywa na Rais Samia kwenye sekta ya Afya hivyo ni vema watanzania wakafanya kitendo cha kizalendo cha kupiga kura October 29
0 Comments