Na Matukio Daima Media
WAUMINI wa dini ya Kiislamu na Watanzania kwa ujumla wamehamasisha kujitokeza kwa wingi hapo Jumatano ya Oktoba 29, 2025 ili kupiga kura na kuwachagua Viongozi sahihi wanaoweza kuwaletea maendeleo sambamba na wote kuwajibika kuitunza amani ya Tanzania.
Wito huo umetolewa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Ali Mbwawa wakati wa Mkutano maalumu wa viongozi na waumini wa dini ya Kiislamu Mkoani Njombe, Mkutano uliofanyika Masjid Taqwa, Mwembetongwa Mjini Makambako, akisema amani ndiyo nguzo muhimu ya maendeleo na ustawi wa Taifa, akiwataka waumini wa dini hiyo kuwa mfano wa kuigwa katika kudumisha utulivu na mshikamano.
0 Comments