Header Ads Widget

UVINZA KUONDOA CHANGAMOTO WANAFUNZI KUKAA CHINI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

HALMASHAURI ya wilaya ya Uvinza imetumia kiasi cha shilingi milioni 139.5 kutengeneza madawati  1987 na ili  kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati kwenye  shule za msingi za halmashauri hiyo kuweza  kuondoa msongamano wa wanafunzi watano kukaa katika dawati moja.

Afisa elimu shule za msingi wa Halmashauri ya wilaya Uvinza mkoani Kigoma, Hilary Bitwaye alisema hayo akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu, Ismail Alli Ussi wakati mwenge wa uhuru ulipotembelea shule ya Msingi Bwawani ambapo kiongozi huyo alikabidhi rasmi madawati 70 kwa shule hiyo ikiwa ni sehemu yaa madawati 1987 yaliyotolewa kwa shule 18 za msingi katika halmashauri hi


Bitwaye alisema kuwa  madawati hayo 1987 yenye dhamani ya shilingi milioni 139.3 yametengenezwa kupitia mapato ya ndani ya halmashauri hiyo lengo likiwa kuboresha mazingira ya kufundishia na ujifunzaji kwa wanafunzi ili kuinua taaluma kwa shule za msingi kwenye halmashauri hiyo.


 Akikabidhi madawati 70 yenye thamani ya shilingi milioni 4.9 kwa uongozi wa shule ya Msingi Bwawani kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Ismail Alli Ussi aliesema kuwa serikali imedhamiria kuendelea kuboresha miundo mbinu katika sekta ya elimu nchini ili wanafunzi wasome kwenye mazingira yenye kuvutia.

Kiongozi huyo wa Mwenge wa uhuru ameipongeza Halmashauri ya wilaya Uvinza kwa kutumia fedha zake za ndani kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo ambao unagusa maisha ya wanafunzi kutoka familia za kawaida na kwamba maboresho hayo yanaacha kumbukumbu kwa wanafunzi hao.


ukiwa wilayani Uvinza mwenge wa uhuru ulitembelea, kukagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi saba yenye thamani ya shiilingi Bilioni 2.4 ukiwemo mradi wa maji wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5 katika kijiji cha Msebehi kata ya Basanza wilaya ya Uvinza ambapo utahudumia wakazi 17,793.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI