Mgombea Urais wa Chama cha Demokratic Party (DP) Juma Abdul Mluya akizungumza na wanachi wa kijiji cha Matyazo kata ya Simbo Halmashauri ya wilaya Kigoma mkoani Kigoma alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni za Urais wa chama hicho.
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mgombea Urais wa Chama Cha Democratic Party (DP) Juma Abdul Mluya amesema kuwa akiingia madarakani atakomesha biashara ya kutoza maiti inayofanywa na hospitali za serikali nchini.
Mluya alisema hayo akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Simbo Halmashauri ya wilaya Kigoma Jimbo la Kigoma Kaskaini na kusema kuwa hospitali kutoza maiti ni kuongeza msiba wa pili kwa wafiwa.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokratic Party (DP) Juma Abdul Mluya (kushoto) akimnadi Mgombea Ubunge wa Chama hicho Jimbo la Kigoma Kaskazini Faraji Kiburwa (kulia) wakati akizungumza na wanachi wa kijiji cha Matyazo kata ya Simbo Halmashauri ya wilaya Kigoma mkoani Kigoma alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni za Urais wa chama hicho.
Akiwa katika ziara ya kampeni ya urais kwa chama chake Mgombea huyo alisema kuwa baada ya mtu kufariki itoshe kumuachia kuwa sadaka ya kumfariji badala ya kumuongezea mzigo wa kudai deni la matibabu huku mtu huyo akiwa na mzigo wa kumsitiri kwa heshima mpendwa.
Sambamba na hilo alisema kuwa suala la wajawazito kujifungua litakuwa bila malipo na mama wajawazito wote watapatiwa vifaa vya kujifungua bure ili kuondoa mzigo kwa familia kuonekana kwamba kujifungua ni suala la anasa.
Wananchi wa kata ya Simbo wakifuatilia mkutano wa Mgombea Urais wa Chama cha Demokratic Party (DP) Adul Juma Mluya
Kutokana na hilo alisema kuwa umefika muda wa CCM kupumzika ili fikra mpya ziweze kuongoza nchi hivyo amewaomba wananchi hao kumpigia kura nyingi mgombea wa chama cha DP siku ya kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu.
Mwisho.
0 Comments