Tumepokea picha za ubora wa juu za setilaiti zinazoonyesha eneo lililoathiriwa na maporomoko ya ardhi yaliyosababisha maafa siku ya Jumapili katika eneo la Darfur magharibi mwa Sudan.
Picha kutoka kwa kampuni maalum ya setilaiti Maxar zilituwezesha kutathmini ukubwa wa maporomoko hayo.
Tumelinganisha picha za setilaiti na video na picha za matokeo ambayo tulithibitisha hapo awali kuwa zilipigwa katika eneo la kusini mwa kijiji cha Tarseen katika milima ya Marra.
Kulingana na uchanganuzi wa Maxar wa picha hizo "mtiririko wa udongo uliotokana na maporomoko ya ardhi inakuonekana kuelekea katikati ya jiji lolote karibu na eneo hilo.
Hii inalingana na kile BBC Verify imekuwa ikiona katika video za baadaye zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii.
Pi inazua maswali kuhusu ni watu wangapi waliofariki, ikizingatiwa kundi la watu wenye silaha linalodhibiti eneo hilo limesisitiza kuwa zaidi ya watu 1,000 walifariki.
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanakadiria kwa uchache watu 370 walifariki lakini wamesema ni vigumu kutathmini ukubwa wa tukio hilo au idadi kamili ya vifo kutokana na ugumu wa kufikia eneo hilo.
Wafanyakazi wa kutoa misaada kutoka mashirika kadhaa wanatarajiwa kufika eneo lililoathiriwa leo Alhamisi.
0 Comments