Header Ads Widget

15 WAFARIKI KATIKA MLIPUKO WA BOMU LA KUJITOA MHANGA NCHINI PAKISTAN

Watu 15 wamefariki na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga karibu na mkutano wa kisiasa nchini Pakistan, mamlaka ilisema.

Mamia ya wanachama wa Chama cha Kitaifa cha Balochistan (BNP) walikuwa wakihudhuria mkutano katika uwanja wa michezo wa Quetta, mji mkuu wa jimbo la Balochistan, wakati bomu lilipolipuka katika eneo la kuegesha magari Jumanne usiku.

Mamlaka za mkoa zilisema Jumatano kwamba idadi ya waliofariki imeongezeka hadi 15.

Kundi la wanamgambo wa Islamic State limedai kutekeleza shambulio hilo.

Balochistan, ambayo inapakana na Afghanistan na Iran, ni eneo kubwa na maskini zaidi nchini humo.

Wakaazi wake pia wanakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa Islamic State na makundi yanayotaka kujitenga.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga hakuweza kufika eneo la mkutano kutokana na ulinzi mkali, waziri wa afya wa Balochistan Bakht Muhammad Kakar alisema, kulingana na mtandao wa Pakistan wa Geo News.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI