Header Ads Widget

NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZAISHAMBULIA BOTI YA MISAADA YA GAZA KATIKA MAJI YA UGIRIKI

 

Watu wakikusanyika karibu na boti kadhaa zinazobeba misaada kwenda Gaza kwenye kisiwa cha Ugiriki cha Syros mnamo tarehe 14 Septemba.

Meli aina ya Flotilla iliyobeba msaada katika Ukanda wa Gaza imeripotiwa kushambuliwa na ndege zisizo na rubani katika maji ya Ugiriki.

Wanaharakati wanaoandaa msaada huo walisema kulikuwa na milipuko na mawasiliano yao yalitatizwa.

Boti hizo hapo awali zilikuwa zimetoka katika bandari ya Uhispania na zilitangaza nia yao ya kuvunja kizuizi cha jeshi la wanamaji la Israeli katika Ukanda wa Gaza.

Sambamba na tukio hili, vifaru vya Israel vimeripotiwa kuingia katikati mwa Mji wa Gaza.

Mashambulizi ya pande zote ya Israel katika mji wa Gaza yamezidisha mzozo wa kibinadamu huko.

Siku ya Jumanne, Rais wa Marekani Donald Trump alikutana na viongozi wa Waarabu na Waislamu katika Umoja wa Mataifa kujadili usitishaji vita huko Gaza, kuachiliwa kwa mateka na utawala wa baada ya vita huko Gaza.

Chombo cha habari cha Imarati kilisema mazungumzo hayo yalilenga katika kumaliza vita, ingawa maelezo ya mpango huo wa Washington bado hayako wazi.

Jana - Septemba 23 - Marais wa Uturuki na Brazil waliikosoa vikali Israel katika hotuba zao kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

"Mashambulizi ya kigaidi ya Hamas hayana uhalali wowote, lakini hakuna chochote kinachohalalisha mauaji ya kimbari huko Gaza," Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, alisema mbele ya Rais wa Marekani Donald Trump katika Umoja wa Mataifa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI