Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Katika kuhamasisha ushiriki wa wananchi kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru September 17 na 18 na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma imeandaa Bonanza la Michezo litakalofanyika Jumamosi, Septemba 6 mwaka huu.
Mkuu wa wilaya Kasulu, Isack Mwakisu alisema hayo akizungumza katika kikao cha maandalizi ya Mwenge kilichokutanisha wadau kutoka sekta za umma na binafsi.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Kasulu amesema bonanza kuwa hilo litakuwa chachu ya mshikamano wa wananchi kuelekea matukio hayo muhimu ya kitaifa.
Alisema kuwa Bonanza hilo litafanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiganamo na litajumuisha michezo mbalimbali ambapo wito kwa Wananchi wote kujitokeza kushiriki.
Mkuu huyo wa wilaya Kasulu alisema kuwa bonanza hilo litaanza kwa matembezi ya pamoja kuzunguka mitaa ya Kasulu mjini na baadaye kurejea viwanja vya Kiganamo kwa michezo na shughuli za kijamii zitakazowaunganisha watu wa kada zote.








0 Comments