Na WILLIUM PAUL, SAME.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Same mashariki kupitia chama cha Mapinduzi, Anna Kilango Malecel amemuomba Mgombea mwenza wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwasaidia kupata wilaya ya kichama Jimbo la Same mashariki.
Anna alitoa ombi hilo jana katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Mgombea mwenza huyo zilizofanyika katika viwanja vya Ndungu wilayani Same ambapo alisema kuwa wilaya hiyo ni kubwa yenye majimbo mawili hivyo viongozi wa chama wamekuwa wakipata shida katika utekelezaji wa majukumu.
Aidha Mgombea huyo alidai kuwa wakata Rais Dkt. Samia anaingia madarakani alikuta jimbo hilo likiwa na vituo vya afya kimoja lakini ameweza kuongeza vituo vinne vya afya.
Alisema kuwa, katika serikali ya awamu ya sita imeanza kujenga barabara ya Same Kisiwani Mkomazi kwa kiwango cha lami ambapo ndicho kilio kikubwa kwa wananchi wa jimbo la Same mashariki.






0 Comments