Muigizaji wa Uingereza Owen Cooper amekuwa kijana mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushinda Tuzo ya Emmy ya muigizaji bora msaidizi.
Cooper, 15, alitajwa kutokana na uhusika wake kama mvulana wa shule anayetuhumiwa kumuua mwanafunzi mwenzake.
Filamu anayoshiriki ya mfululizo wa sehemu nne pia imechukua tuzo la filamu bora, pamoja na uelekezi na uandishi bora, na tuzo za uigizaji za Stephen Graham na Erin Doherty.
Katika hotuba yake ya kukubalika tuzo yake, Cooper alisema: "Kusimama hapa ni jambo jema sana...
"Nilipoanza masomo haya ya maigizo miaka kadhaa nyuma, sikutarajia hata kutambulika Marekani, licha ya hapa."
Cooper, ambaye aliigiza kama kijana Jamie Miller, alisema: "Nadhani usiku wa leo unathibitisha ikiwa unasikiliza, na unazingatia na kujituma, unaweza kufikia chochote maishani.






0 Comments