Header Ads Widget

BASHUNGWA AWAAHIDI MAJI NA UMEME WANANCHI WA KIJIJI CHA KANOGO_NYAKABANGA IKIWA NI MWENDELEZO WA KAMPEINI ZAKE JIMBO LA KARAGWE

 

Na Matukio daima media

Mgombea Ubunge  Jimbo la Karagwe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Innocent Bashungwa, ameendelea na mikutano ya kampeni zake   katika Kijiji cha Kanogo, Kata ya Nyakabanga, Wilaya ya Karagwe.

Katika mkutano huo, Bashungwa ameahidi wananchi huduma ya maji safi kwa kuchimba visima kupitia mitambo ya Wizara ya Maji ambapi  ameweka bayana dhamira ya Serikali  ya kufikisha umeme katika vitongoji vyote vya kijiji hicho ili kuongeza tija katika shughuli za kiuchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi.

Bashungwa amesisitiza umuhimu wa  wananchi kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025 kwa kujitokeza  kwa wingi na kuwachagua kwa kishindo Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge pamoja na Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi ili kuendeleza maendeleo ya Taifa.

Kampeni hizo zinazofanyika ngazi ya vijiji zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Karagwe, Paschal Rwamugata.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI