Mahakama ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida imemhukumu Paul Petro Luluu (30), mkazi wa Kijiji cha Nkonko kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Itika Koroso baada ya upande wa mashitaka kuthibitisha tukio hilo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2022 na Juni 29, 2025, katika Tarafa ya Nkonko, Wilaya ya Manyoni.
Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani, tukio hilo lilifichuliwa baada ya raia wema kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, ambalo liliendesha upelelezi, kukamata mtuhumiwa na kumfikisha mahakamani.
0 Comments