Na Mwandishi Wetu, Dar
Mwandaaji na mtayarishaji wa vipindi wa Makampuni ya IPP MEDIA, ITV na Radio One, Aboubakar Sadik amenusurika kifo baada ya gari yake kuteketea kwa moto majira ya saa Sita usiku wakati akitokea kazini kwake Mikocheni Jijini Dar es salaam.
Tukio hilo limetokea usiku huu wa majira ya saa sita September 2, 2025 ambapo katika kurasa zake za Kijamii, Aboubakar Sadik ameweza kupost gari yake hiyo ikiwa inawaka moto na baadae kuungua kabisa.
"Alhamdulillah....Nimeunguliwa na gari usiku huu nikitoka kazini, Mungu mkubwa nipo salama." Aliweka ujumbe huo pamoja na picha mjongeo ya gari hiyo ikiwaka moto.
Ambapo baadae aliweza kubandika bandiko lingine pamoja na gari hilo likiwa limeteketea kabisa ujumbe:
"Sifa na utukufu ni kwa Mola wetu, Alhamdulillah".
![]() |
Muonekano wa gari hiyo |
0 Comments