Mahakama nchini Thailand imemuondoa madarakani Waziri Mkuu nchini humo Paetongtarn Shinawatra kwa sababu ya simu iliyovuja na aliyekuwa kiongozi wa Cambodia Hun Sen.
Waziri huyo alimpigia simu Hun Sen na kumuita "mjomba" kisha akazungumza vibaya kuhusu kamanda wa jeshi la Thailand.
Wakosoaji walimshtumu kwa kudhoofisha jeshi lenye nguvu la Thailand.
Paetongtarn aliomba msamaha baada ya kuvuja kwa simu hiyo, akidai ilikuwa "mbinu ya mazungumzo" huku kukiwa na mvutano mbaya wa mpaka na Cambodia.
Lakini Mahakama ya Kikatiba ya Thailand leo imetoa uamuzi kwamba "vitendo vyake vilikinzana na fahari ya taifa na kuzingatia maslahi ya kibinafsi zaidi ya nchi, ambayo ilikiuka kabisa au kushindwa kufuata viwango vya maadili vilivyowekwa"
Katika maoni yake ya kwanza baada ya uamuzi huo, Paetongtarn alikiri uamuzi huo, lakini akasema kwamba umesababisha "mabadiliko mengine ya ghafla" nchini Thailand, ambapo anakuwa kiongozi wa tano tangu 2008 kuondolewa madarakani na mahakama.
Naibu Waziri Mkuu wa Thailand sasa atachukua nafasi ya Paetongtarn kabla ya kura mpya kufanyika kumchagua waziri mkuu mpya.
0 Comments