Header Ads Widget

WATU SITA WAFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE NDOGO YA KIMATIBABU KENYA

 

Watu sita wamefariki baada ya ndege ndogo ya shirika la misaada ya matibabu kuanguka katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kulingana na afisa wa eneo hilo.

Charity Amref Flying Doctors walisema kuwa ndege ya Cessna ilipaa kutoka uwanja wa ndege wa Wilson siku ya

Alhamisi alasiri na ilikuwa ikielekea Hargeisa nchini Somalia ilipoanguka na kuwaka moto katika jengo la makazi eneo la Githurai Nairobi.

Kamishna wa Kaunti ya Kiambu Henry Wafula alisema watu wanne waliokuwa kwenye ndege hiyo waliuawa, wakiwemo madaktari, wauguzi na rubani wa ndege hiyo - pamoja na watu wengine wawili waliokuwa chini, huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya.

Wachunguzi wametumwa kwenye eneo la ajali ili kubaini chanzo chake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI