Header Ads Widget

AUSTRALIA YATOA WITO KWA ISRAEL KUTOITEKA GAZA CITY

 

Tunapata hisia zaidi za kimataifa kuhusu mipango ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ya kuudhibiti mji wa Gaza.

Penny Wong, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, ametoa taarifa akisema "Australia inatoa wito kwa Israel kutofuata njia hii, ambayo itazidisha maafa ya kibinadamu huko Gaza."

Alisema uhamisho wa kudumu wa kulazimishwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na wito wa mara kwa mara wa kusitishwa kwa mapigano, misaada itiririke bila kuzuiliwa na kundi la wanamgambo wa Hamas kuwarudisha mateka waliochukuliwa Oktoba 2023.

"Suluhu ya mataifa mawili ndiyo njia pekee ya kupata amani ya kudumu - taifa la Palestina na Taifa la Israel, wanaoishi bega kwa bega kwa amani na usalama ndani ya mipaka inayotambulika kimataifa," aliongeza.

Waziri wa Mazingira wa Australia Murray Watt hapo awali pia alitoa ukosoaji wake, akisema serikali "ilipinga vikali uvamizi wa Gaza kwa nguvu".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI